Heshimu Kila Mtu!!!

"Treat people humanily, irrespective of their appearance, wealth and status." //  "Hudumia watu kibinaadamu, pasipo kuangalia muonekano wake, heshima yake na hadhi yake."

Katika maisha tunakutana na watu wengi sana wapo ambao wapo chini yetu na wapo ambao wametuzidi kiuwezo, inaweza kuwa kwa namna yoyote ile. Utu wa mwanaadamu onekana si kwa mali yake au kitu chochote kile alichonacho bali utu wa mtu unaonekana kwa namna anavyoishi na watu wengine ikiwemo watu wanaomzunguka. Ukiishi vizuri na watu wengine basi watu hao watakupenda na kukuheshimu kwasababu wewe pia unawaheshimu. Kuna msemo unasema "Usipoteze watu kwasababu umepata mali kwani njia ya kupata mali ni kwa kupata watu." msemo huu una maana kubwa sana kama mtu utaishi na watu wengine vizuri kisha ukaanzisha kitu chako mfano ni biashara basi wale watu ulioishi nao vizuri ndio watakuwa watu wa kwanza kutumia bidhaa au huduma yako na kuwa wateja wako wazuri pia kukusaidia kuongeza idadi ya wateja wako. Ni muhimu sana kuwa mtu ambaye unaishi vizuri na jamii yako. Bofya hapa kusoma umuhimu wa kuishi na watu vizuri. Kuishi vizuri na watu kuna faida kubwa sana, anza sasa kuishi na watu na wao wataishi na wewe vizuri. Kumbuka Inawezekana.

Comments