"Every man has a key to his heart, and knowing his personality assists in identifying the right key to open it." // "Kila mtu anafunguo katika moyo wake, na kujua yeye ni mtu wa namna gani kutakusaidia kujua funguo sahihi ya kuufungua."
Kila binaadamu ana mambo ambayo yeye binafsi anayapenda yani mambo ambayo akifanyiwa basi hujiona ni mtu mwenye furaha sana. Vitu hivi tunaviita funguo za moyo yani mambo ambayo mtu akifanyiwa basi moyo wake hufunguka. Ukweli ni kwamba watu wengi hawatambui funguo za mioyo ya watu wanao wazunguka mfano mtu ana kuwa na rafiki lakini hajui ni njia gani anaweza kutumia kufungua mioyo ya rafiki wake. Njia ya kujua funguo za moyo wa mtu wa karibu yako ni kwa kufanya utafiti juu yeye ukajua ni mtu wa namna gani, baada ya hapo utaweza kufahamu njia na namna za kutumia kufungua moyo wako. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment