Jambo La Kufanya Ili Ufanikiwe!!!

"If You Would Like To Be A Head Instead Of A Tail,Then Eagerly Try To Practise All Skills Regardless Of What They May Be." // "Kama Unataka Kuwa Kichwa Badala Ya Mkia,Basi Kuwa Na Shauku Ya Kufanyia Mazoezi Mbinu Zote Bila Kujali Zitakuwa Zipi."
Watu wengi wanataka kufanikiwa katika mambo mbalimbali katika maisha yao.Watu hawa wanaotaka kufanikiwa wapo ambao wanatamani tu kufanikiwa lakini hawa fanyi kitu chochote kuliendea lile wanalolitaka,na wapo ambao wanatamani kufikia sehemu fulani katika maisha yao na kila siku wanajaribu kufika kule wanapotaka kwenda.Kuna mtu alisema "If You Want To Be Successful As Bad As You Want To Breath Then You Will Be Successfull" // "Kama Unataka Kufanikiwa Kama Vile Unavyotaka Kupumua Basi Utafanikiwa." Watu wanatamani tu siku moja ni fike sehemu fulani au ni pate kitu fulani ila kila siku zinapo zidi kwenda mtu yule anaishia tu kutamani na hachukui hata hatua moja ya kufika kule anapotaka kwenda,watu wanamna hii ni watu ambao wanapenda kuhairisha mambo au ni watu ambao waoga wakujaribu mambo mbalimbali kwasababu wanahofia watafeli au watachekwa na watu na kuishia kutopigania ndoto zao.Leo naomba ni kwambie ya kuwa "Procrastination Is The Death Of Success." // "Kuhairisha Ndio Kifo Cha Mafanikio Yako."  Bofya Hapa Kujifunza Mambo Yanayokufanya Uwe Ni Mtu Wa Kuhairisha. Kama unataka kufanikiwa na unataka usiwe mkia na uwe kichwa basi jitahidi kujifunza mambo mbalimbali au mbinu mbalimbali zitakazo kuwezesha kufika kule unapotaka kwenda.Unaweza ukajifunza mbinu mbalimbali mfano kama wewe ni mfanya biashara ungependa kuongeza mapato yako basi unaweza kutafuta Mentor au ukasoma Vitabu mbalimbali au hata kuudhuria Semina mbalimbali za biashara ili kujifunza mbinu na mambo mengine zaidi.Kumbuka ukiwa ni mtu wa kupenda kuongeza maarifa katika jambo unalolifanya basi itakuwa ni jambo la muhimu kwako kwani utaongeza Thamani ambayo itakutofautisha wewe na watu wengine,na ukiwa mtu unayependa kuongeza thamani katika mambo unayofanya basi mambo yako yatakuwa ni mambo yenye ubora kuliko wengine.

Mfano wa umuhimu wa kuongeza thamani ni kama huu "Mtu anaweza akafungua duka katika mtaa mmoja ambao una maduka mengi mfano sehemu ya kuuzia chips ila wenzake hawana sehemu ya kukaa wateja ila yeye anayosehemu ambayo watu wanaweza kukaa na kula vizuri,sehemu hii wanaweza kupata wateja wengi kwasababu wao waliamua kuongeza thamani katika jambo wanalofanya na kuweza kujitofautisha na wengine.Kuna mtu aliwahi kusema "We Are Not Payed for The Time That We Spend But We Are Payed For The Value That We Bring In The Time That We Spend." // "Hatulipwi Kutokana Na Muda Tunaotumia Bali Tulipwa Kutokana Na Thamani Tunayotoa Katika Muda Tunaotumia." Mfano mzuri wa kuonyesha umuhimu wa maneno haya ni katika mpira,wachezaji katika mpira wanacheza pamoja lakini kila mchezaji analipwa tofauti na mwengine sio kwasababu wanacheza sana, hapana ila ni kwasababu mchezaji mwengine ana ongeza thamani katika uchezaji mpira wake na kufanya alipwe tofauti na wengine.Kumbuka Inawezekana.

Comments