Makosa Wajasiriamali Wanatakiwa Wa Yaepuke!!!

Makosa 5 Wajasiriamali Wanatakiwa Wayaepuke.
Katika safari yako ya ujasiriamali kuna makosa mengi sana ambayo utayafanya hadi kufikia kule juu unapopataka. Ni muhimu sana kuchulia makosa hayo kama mafunzo na changamoto na kuendelea nayo. Leo tutazungumzia makosa 5 ambayo unatakiwa uyaepuke kama mjasiriamali.

1.) Kuongea na kutokufanya.
Wajasiriamali wengi wanapenda kuongelea tu kuhusu mipango yao ya kibiashara na wanashindwa kabisa kuyatekeleza kivitendo. Ukweli ni kwamba mipango uliyonayo kuhusu biashara yako haiwezi kutekelezeka kwa kuongea bali yanatekelezeka kwa kufanya.

2.) Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
Wajasiriamali wengi wanapenda kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Unaweza kumkuta mjasiriamali baada ya kufocus kwenye biashara yake anaweza kukaa na kufanya jambo lengine ambalo si la biashara yake ambalo si jambo sahihi.

3.) Kuwa ajiri watu ambao si sahihi.
Katika mambo ambayo kama mjasiriamali unatakiwa kuwa makini nayo sana ni sehemu ya watu ambao watakuwa wanakufanyia kazi. Katika biashara yako hakikisha unafanya kazi na watu sahihi ambao wana uwezo wa kufanya kazi unayotaka wewe wafanye.

4.) Kupanuka haraka.
Katika jambo ambalo unatakiwa uwe makini nalo sana ni katika sehemu ya kupanua biashara yako pale inapokuwa. Usipanue biashara yako haraka sana kwani inaweza kupelekea kuanguka kwa biashara yako kama huna mipango mizuri.

5.) Kutojiamini wewe mwenyewe.
Kama unataka ufanikiwe kibiashara basi amini kama unaweza amini katika mawazo yako. Amini ya kuwa biashara au wazo ulilo nalo linaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kama utajiamini na kusimamia mawazo yako.
Kumbuka Inawezekana.

Comments