Sababu Iliyomfanya Henry Ford Kuwa Tajiri Mkubwa!!!

"Henry Ford is a success, because he understands, and applies the principles of success. One of these is DESIRE: knowing what one wants." // " Henry Ford ni Mafanikio, kwasababu anaelewa, na anafanyia kazi kanuni za mafanikio. Moja ya haya ni HAMU: kujua nini mtu anataka."

Henry Ford alikuwa ni mtu tajiri sana katika nchi ya Marekani. Alikuwa ni mmiliki wa kampuni ya magari. Tajari huyu alikuwa ana vitu mbalimbali ambavyo vilimfanya awe tajiri mkubwa moja wapo ni alikuwa ni mtu asiyekubali kukata tamaa wala hakubali kukatishwa tamaa. Aliamini katika kile anachofanya aliamini katika mawazo yake na kwamba kile alichotaka kufanya alikubali kuendelea nacho mpaka kifike levo ya kufanikiwa au kutokea. Katika siku yako ya leo kama una mawazo au ndoto ambayo ungependa itokee basi pambana na ndoto yako pigania ndoto yako mpaka uone ya kwamba imetokea. Usikate tamaa hata kama utakutana na changamoto ya aina gani endelea kupambana na kupigania ndoto ya maisha yako ambayo wewe unaiamini. Kumbuka Inawezekana.

Comments