Sababu Ya Makampuni Makubwa Kufa!!!

"Makampuni makubwa yanaenda polepole kwasababu mawazo mazuri yanapotea kwasababu yanapitia mchakato mrefu mpaka kukubaliwa."  Kampuni ya Nokia ilikuwa ni kampuni bora na kubwa sana duniani iliweza kutengeneza bidhaa bora lakini kutokana na kushindwa kuenda na kasi ya uvumbuzi duniani soko la Nokia lilikuja kufa na kupotea kabisa.
Kampuni nyingi hufa kutokana na kukosa ubunifu ambao husaidia kuendesha kampuni kuwa inayoenda na wakati. Makampuni makubwa yanatakiwa kufanyia kazi ushauri wa wateja wao pamoja na wafanyakazi wao. Ushauri wa mtu wa nje unaweza kuonekana kama ushauri ambao sisahihi kwa biashara yako lakini chukua ushauri unaopewa na kuuchunguza kama ni sahihi kwenye biashara yako. Kumbuka jifunze kupitia wateja na wafanyakazi wako. Kumbuka Inawezekana.

Comments