Umuhimu Wa Kuweka Malengo Kwa 2019!!!

Andrew Carnegie anasema "If You Want To Be Happy,Set A Goal That Commands Your Thoughts,Liberates Your Energy And Inspires Your Hope." // "Kama Unataka Kuwa Na Furaha,Weka Lengo Ambalo Linaamrisha Fikra Zako,Linaokoa Nguvu Yako Na Linahamasisha Matumaini Yako." 
Vijana wengi sana hatujui umuhimu wa kuweka malengo katika maisha yetu.Unaweza kumuuliza mtu una malengo gani katika maisha yako au unatafuta nini katika maisha au unataka kuwa nani? Unakuta kijana hawezi kujibu maswali haya.Leo nataka kukwambia ya kuwa bila malengo hauna unapoelekea kwasababu hujui unaenda kufanya nini na wapi.Maisha ni kama mfano wa safari jinsi utakavyoiyanda safari yako ndivyo itakavyo kuwa wepesi wa safari yako.Kama wewe katika safari yako ya maisha hauna malengo au hujui unataka kuwa wapi katika maisha yako au ufanye nini katika maisha yako basi utaishi maisha yako bila kujua unataka nini na umeamua nini katika maisha unayoishi.Malengo ni kitu cha muhimu katika maisha yako na katika mambo unayofanya uwe umeajiriwa,umejiajiri au mwanafunzi kitendo cha kuweka malengo na kuwa na malengo katika jambo lako ni jambo lililo kuwa la muhimu kwani ndio litakalo kujulisha umetoka wapi na unataka kwenda wapi."Life Without Goals Is Like An Empty Cup" // "Maisha Bila Malengo Ni Kama Kikombe Kitupu." Kama hutaweka malengo katika sehemu mbalimbali za maisha yako basi itakuwa kila siku unafanya vitu vilele visivyo kuwa na tofauti au kuleta tofauti katika maisha yako.Tuchukue mfano wa mfanya biashara ambaye hana malengo katika biashara yake yani yeye anafanya biashara ili tuapate hela hata kama atakuwa palepale miaka nenda miaka rudi,mfanya biashara huyu atakuwa anafanya biashara isiyo kuwa na ramani ya kukuwa zaidi na kuendelea mbele kwasababu biashara hii ni biashara inayoendeshwa bila malengo.Kuna sababu sita (6) za wewe kuweka malengo katika maisha yako:
1)Goals Propel You Forward(Lengo Linakusukuma Kwenda Mbele):Ukiweka malengo katika maisha yako basi hayo malengo yatakuwa chachu ya wewe kuendelea mbele katika maisha yako,maana unajua kuna lengo ambalo ninataka kulitimiza.
2)Goals Transform Insurmountable Mountains Into Walkable Hills(Malengo Hubadilisha Milima Isiyoweza Kupandika Kuwa Ni Milima Midogo Inayoweza Kupandika):Mtu mwenye kutamani mambo makubwa huona hawezi kuyafikia mambo hayo na hubaki kutamani tu ila mtu mwenye malengo huyaendea malengo yake hata kama ni makubwa kidogo kidogo mpaka kuyafikia,kuna mtu aliwahi kusema "The Person Who Removes A Mountain Begins By Carrying Away Small Stones." // "Mtu Anayeondoa Mlima Anaanza Kwa Kubeba Mawe Madogo."
3)Goals Help Us Believe In Ourselves(Malengo Yanatusaidia Kujiamini):Ukiwa na lengo katika maisha yako au kazi yako au hata masomo yako yanakufanya uwe ni mtu unayejiamini kwasababu unajua kila siku unapiga hatua fulani kulifikia lengo lako Theodore Roosevelt aliwahi kusema "Believe You Can And You're Halfway There."// "Amini Unaweza Na Umebakisha Nusu Kufika Huko Unapotaka Kuwa."
4)Goals Hold You Accountable For Failure( Malengo Ya Takufanya Uwajibike Na Kutoweza):Kufeli ni jambo la kawaida katika kuyaendea malengo yako, ukiwa na malengo ukifeli ya takufundisha ni kitu gani uboreshe katika kulifikia lengo lako.
5)Goals Tell You What You Truly Want(Malengo Yanakwembia Unataka Nini):Mtu aliyejiwekea malengo anajua anataka nini katika maisha yake.Maisha ni kama safari ukijua unasafiri kwenda kufanya nini basi utajua dhumuni lako na kukimbilia safari yako.
6)Goals Make You Live Life To The Fullest(Malengo Ya Takufanya Uishi Maisha Kwa   Kwa Ukamilifu):Ukishapanga lengo lako basi utaishi maisha yako ukiwa unalengo ambalo unaliendea katika maisha yako huku ukiwa hukati tamaa katika maisha yako.Kwasababu unajua kuna lengo ambalo unaliendea na unatamani siku moja litimie.
Brian Tracy akasema "Goals Without A Plan Is Just A wish." // "Malengo Bila Mipango Ni Kama Kutamani."  Kama utaweka malengo yako pasina kuwa na mipango ya kufikia malengo yako basi malengo yako yale yatakuwa kama jambo unalolitamani tu nasio unalolitaka kuna mtu aliwahi kusema "Wishes Will Not Take You Anywhere Only Goal Will Take You Where You Want To Be." // "Kutamani Hakuta Kupeleka Kokote Malengo Ndiyo Yatakayo Kupeleka Kule Unapotaka Kuwa." 
Mipango ni kitu cha muhimu katika kufikia malengo yako uliyopanga.Mipango ndio ramani itakayo kuonyesha wewe ni kwa namna gani utafikia malengo yako uliyojiwekea.Katika kufikia malengo yako ni lazima ujue utumie mbinu gani kufike kule unapotaka kuwepo.Unaweza ukatumia mbinu mbalimbali kutokana na malengo uliojiwekea.Mfano kwa mwaka huu umejiwekea lengo la kuacha tabia ya kuhairisha mambo unaweza ukatumia mbinu ya kusema kwa kuwa ninataka kuacha tabia ya kuhairisha mambo basi nitatumia mpango wa kutopoteza muda katika maisha yangu ya kila siku.Au kama umepanga mwaka huu unataka unyanyue biashara yako unaweza ukasema kwa kila mshahara nitakao pata katika biashara yangu basi nitaweka kiasi kidogo kama akiba ambayo utakuwa mtaji baadaye katika kukuza biashara yangu.Malengo tofauti tofauti yanahitaji mipango tofauti tofauti ili ku ya fikia.Hakikisha mipango unayoweka isiwe ni mipango itakayotesa au kuumiza wengine.Kumbuka Inawezekana

Comments