Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini watu wengi wanakata tamaa au ni kwanini wewe binafsi kuna muda unafika unashindwa kabisa kuendelea na kukata tamaa.
Moja ya sababu kubwa ambayo ina wafanya watu wakate tamaa ni pale mambo waliyoyatarajia kuyaona au kuyapata yanapokuwa hayaonekani, kwa maana nyengine ni pale wanaposhindwa kuona matokeo ya mambo wanayoyafanya. Ukweli ni kwamba katika maisha sikila mpango utakao panga basi ni lazima utokee kama vile wewe ulivyopanga muda mwengine mambo hayatokei kama ulivyopanga kwasababu maalumu mfano unaweza kusema leo nitakapo fika eneo langu la kazi nitafanya jambo fulani ambalo kwa hakika litaleta matokeo fulani lakini kadiri muda unapozidi kwenda unaona mbona mambo hayatokei na mwishowe unakataa tamaa. Leo naomba ni kwambie ya kuwa katika mipango yako unayoipanga kuna mipango ambayo itachukua muda mrefu sana mpaka ilete matokeo na muda mwengine kuna mambo ambayo unaweza ukapanga yakaleta matokeo ya haraka sana. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwa mvumilivu katika mipango unayoipanga na ujue si kila mpango utaleta matokeo chanya. Endelea kupambana kwa ili ufikie malengo yako ni muhimu sana kutokata tamaa hasa katika nyakati ngumu. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment