Jack Canfield says "If you are clear where you are going and you take several steps in that direction every day, you eventually have to get there. If I head north out of Santa Barbara and take five steps a day, eventually I have to end up in San Francisco. So decide what you want, write it down, review it constantly, and each day do something that moves you toward those goals." // Jack Canfield anasema "Kama unajua wapi unataka kwenda na unachukua hatua kila siku kwenda kwenye hilo jambo, basi hivi karibuni utafika. Kama nitakwenda nje ya Santa Barbara na kuchukua hatua 5 kila siku, basi nitafika San Francisco. Kwa hiyo chagua nini unataka, kiandike, kiangalie kila mara na kila siku fanya kitu kitakacho kufikisha kule kwenye malengo yako."
Katika maisha yako kuna mambo mengi sana unapitia. Katika maisha kama huna dira ambayo itakuongoza nini cha kufanya basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuangaka kwasababu hujui unapokwenda. Dira ya maisha yako ni malengo ambayo wewe unajiwekea ambayo unataka kila siku uyaone yametimia. Ni muhimu sana kufatilia malengo yako na kuhakikisha kila siku unapiga hatua moja kuyafikia. Niambie kwenye comment unatumia njia gani kufikia malengo yako. Share na marafiki zako ISA APP na wao waweze kujifunza kama wewe. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment