Moja ya jambo ambalo ni muhimu sana kwa mjasiriamali yeyote yule ni kuwa na elimu juu ya biashara anayoifanya.
Watu wengi wanaofanya ujasiriamali wanaona kuwa na elimu juu ya ujasiriamali sio jambu la muhimu katika kufanya ujasiriamali. Ukweli ni kwamba elimu ya ujasiriamali inaweza sana kusaidia kufanya ujasiriamali kwa umakini zaidi na kwa uelewa ukubwa wa ujasiriamali. Unaweza kupata elimu ya ujasiriamali kupitia vitabu, semina, wafanya biashara, taasisi zinazofundisha ujasiriamali na kadhalika. Kuwa na elimu juu ya biashara kutakusaidia sana kuweza kufanya biashara yako kwa uwezo mkubwa sana na utaweza kujitofautisha na wengine. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment