Kuna msemo unasema ''ALL ACHIEVEMENT, ALL EARNED RICHES, HAVE THEIR BEGINNING IN AN IDEA!'' // ''MAFANIKIO YOTE, UTAJIRI WOTE ULIOPATIKANA, UNA MWANZO WAKE KATIKA WAZO."
Umeshawahi kujiuliza kwanini mtu fulani anaingiza pesa nyingi kuliko mimi? Na je uliwahi kujiuliza pesa hizo nyingi chanzo chake ni nini? Ukweli ni kwamba biashara nyingi ambazo zinaingiza pesa nyingi hapa duniani mwanzo wake ulikuwa ni wazo. Mfano mzuri ni hapa Tanzania angalia biashara nyingi zilianza kama wazo na baadaye hilo wazo lilifanyiwa kazi na kuwa wazo halisi. Je wewe unawaza mawazo mangapi kwa siku, wiki, mwezi au hata mwaka? Na je umewahi kujiuliza je nifanye nini ili niweze kubadilisha maisha yangu kwa kutumia mawazo yangu. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment