Faida Za Kukubali Kukataliwa.

Kuna msemo unasema "The FEAR OF CRITICISM is at the bottom of the destruction of most ideas which never reach the PLANNING and ACTION stage." // "Woga wa KUKATALIWA ndio ambao upo juu katika kuharibu mawazo ambayo haya kufika nafasi ya kupangwa au kuchukuliwa hatua."

Watu wengi wamekuwa wa kishindwa kuishi maisha yao kutokana na woga wa kukataliwa na watu. Mfano mtu anataka kuanza jambo lake lakini anawaza fulani atanifikiria vipi au ndugu zangu watasemaje au hata marafiki watasemaje. Mawazo haya yamekuwa ni chanzo kikubwa sana kilichofanya watu wengi kukosa kuishi maisha ambayo walitakiwa kuishi kama wanavyotakiwa kuishi. Ukweli ni kwamba kila binadamu ana mtazamo tofauti kuhusu maisha saa nyengine kile kilicho bora kwako kina weza kisiwe bora kwa mwengine na kilicho bora kwa mwengine kina weza kisiwe bora kwako. Anza sasa kufanyia kazi mawazo yako na uache kufikiria watu watasema nini kuhusu mimi. Kumbuka Inawezekana.

Comments