"Where failure is experienced, it is the individual, not the method, which has failed. If you try and fail, make another effort, and still another, until you succeed." // "Ambapo kuanguka panapatikana, ni mtu, na sio njia iliyofeli. Kama ulijaribu na ukafeli, fanya juhudi tena, tena nyengine, mpaka ufanikiwe."
Katika maisha yako kuna nyakati utaanguka na kupoteza muelekeo kabisa. Ukikata tamaa nyakati kama hizo utakuwa umeruhusu ndoto zako zisiwe zenye kutimia. Nyakati kama hizo ndio nyakati za kusimama na kumuomba Mungu akupe nguvu ya kuendelea mbele. Usikubali kukatishwa tamaa na mtu mwengine. Pambana na pigania ndoto ya maisha yako. Kumbuka Inawezekana.

Comments
Post a Comment