Faida Za Kuongeza Thamani Katika Biashara.!!!

"Kuna tofauti kati ya kutengeneza thamani na kufikisha thamani."
Biashara yoyote ile ili ifanikiwe na kuendelea juu basi inatakiwa iwe ni biashara inayotoa thamani kwa wateja wako. Thamani ndiyo inayokutofautisha kati ya wewe na washindani wako. Kama biashara yako iko mtandaoni kwa mfano, basi kama utataka ifanikiwe na kufika juu basi unatakiwa uongeze thamani kwenye eneo lako la usafirishaji. Katika eneo hili unaweza kujitofautisha na wenzako kwa kuongeza urahisi wa bidhaa kumfikia mteja pamoja na ulinzi wa bidhaa za wateja wako. Katika kila eneo la biashara yako angalia sehemu ambayo unaweza kuongeza thamani na ufanye hivyo. Kumbuka Inawezekana.

Comments