Ukweli Kuhusu Ujasiriamali!!!

Hivi umeshawahi kujiuliza ni nini maana sahihi ya ujasiriamali? Najua umeshawahi kupata majibu mengi sana kuhusu maana ya kitu hiki wengine wanasema ujasiriamali ni kuuza na kununua na wengine husema ni kununua na kuuza kwa bei ya juu ili kupata faida.Ukiangalia hapa unaweza kuona hizi maana zote ni sawa ila leo naomba ni kwambie maana halisi ya ujasiriamali.Neno ujasiriamali lina maneno mawili yani  Ujasiri pamoja na Mali.Ili uweze kuwa mjasiriamali mzuri unatakiwa uwe Jasiri na uwe na Mali hata kama mali hiyo itakuwa kidogo kiasi gani.Maana ya ujasiriamali ni kitendo cha kutengeneza sio sayansi ni sanaa,ni sanaa ya kutengeneza huduma au bidhaa ili majirani,ndugu na marafiki waweze kununua.Kama sanaa yoyote ile ni lazima ifundishwe na kufurahiwa.
Katika maana hii ya ujasiriamali tunaona ya kuwa ili mtu aweze kuwa mjasiriamali mwenye tija au mwenye mafanikio basi hana budi ila kutumia ubunifu katika biashara yake anayofanya.Tafuta njia mpya na buni mambo mapya ambayo yatakayo tofautisha kati ya biashara yako na biashara za watu wengine na ukifanya hivyo basi biashara yako itakuwa ni biashara ya mafanikio.Ukitaka kudumu katika biashara basi kuwa mbunifu. Kumbuka Inawezekana.   

Comments